Friday, April 17, 2015

STORI YA KWELI KUHUSIANA NA KIJANA JAPHET

ALITOLEWA KAFARA NA BABA YAKE MZAZI ILIAPATE UTAJIRI, ALIFUKIWA NDANI YA KICHUGUU NA KUBADIRISHWA NGOZI YAKE KAMA GAMBA LA NYOKA.

Askofu Daniel Ouma(Dao) mwenye suti nyeusi na chupa ya mafuta ya Upako(Anointing oil) mkononi wa kanisa la bonde la baraka lililopo Musoma akimfanyia maombezi kijana Japhet mwenye tisheti ya buluu ambae ameweka mikono yake usoni.



 Kijana Japhet alikuwa akiishi jijini Dar eslaam na wazazi wake wote, baba yake japhet aliingiwa na tamaa ya utajiri ndipo akaenda kwa mganga wakienyeji ili apatiwe mbinu za kupata utajiri, mganga alimwambia kuwa ili apate utajiri nilazima atoe kafara mtoto wake ndipo apate utajiri.

Ndipo aliamua kumtoa kafara kijana wake Japhet ili kusudi apate mali kama alivyo kuwa amekusudia lengo ikiwa ni kuondokana na umaskini wakukosa fedha na malizingine nyingi. Kijana Japhet anasimulia jinsi alivyotolewa kafara na baba yake mzazi japo Mungu alisimama upande wake kupitia maombi ya Askofu Daniel Ouma(Dao) wa kanisa la Bonde la Baraka ambako kijana japhet aliponywa kinabii.

Kijana Japhet  akielezea ‘’Ilikuwa ni mara ya pili kwa baba yangu mzazi ambae aliamua kunitoa kafara ili atajirike,awali baba yangu alimtoa kafara kaka yangu ambae siwezi kumtaja jina lake, kaka alikufa japo baba hakupata mali kama ambavyo alikuwa ameambiwa na mganga wake’’Mtoto Japhet  aliendelea akisema kuwa ‘’Baada ya mpango wake huo kukwama ndipo aliambiwa atoe kwa mara ya pili kijana wake, Ngozi yangu ilibadirishwa na kuwa gamba la nyoka kisha akafukia nyoka kwenye kichuguu ili yule nyoka anapojivua gamba nami ngozi yangu inabadilika kuwa gamba la nyoka huyo, ngozi ya mwili wangu ili badilika kabisa nikawa siwezi hata kuvaa nguo, kwani kila nilipo jaribu kuvaa mavazi yalinata kwenye mwili wangu na kupelekea mavazi yale kushikamana na mwili wangu’’

SAFARI YA UPONYAJI WA KIJANA JAPHET NDANI YA BONDE LA BARAKA KWA MATAIFA YOTE MUSOMA.

Askofu Daniel Ouma (Dao) akiwa ameshikilia mkono wa kijana Japhet kwa ajili ya kumfanyia maombezi pichani, Kijana japhet mkono wake unaonekana ukiwa umebanduka ngozi kutokana na baba yake mzazi kumtoa kafara ili apate utajiri.










Pia baadhi ya viungo vya mwili wangu vilianza kufifia kama vile kucha, vidole, nilikuwa nikiishi kwa shida sana na nilikosa amani wakati wote, nilikuwa nikizungukwa na nzi wengi kila wakati ilifikia hatua nikawa nanuka sitamaniki mbele za watu wengine huku wengine nikiwaona wakifurahi na kurukaruka wakiwa na afya njema’’

‘’Mama yangu mzazi baada ya kugundua kwamba nimeshatolewa kafara na muda wowote naweza kufa, aliamua kunitorosha kutoka jijini Dar eslaam na kunileta musoma kwa ndugu yake mama, ambapo baada ya kufika mjini Musoma mama aliendelea kutafuta mbinu ya kunipatia matibabu, alifika kwa watumishi wengi sana wa Mungu baadhi yao waliponiona jinsi nilivyo waliogopa hata kunifanyia maombezi kwani sikutamanika machoni pa watu wengi wao walikuwa wanamwambia mama kuwa nakufa kweli mama yangu alikuwa na mawazo kila wakati huku akiwaza jinsi gani anaweza kuninusuru na roho ya mauti ambayo ilikuwa tayari inaniandama baada ya kuona hali hiyo inazidi kuwa mbaya kila wakati mama aliambiwa na watu kwamba nipelekwe kanisa la bonde la Baraka kwa mataifa yote nitapona kutokana na Askofu huyo kutajwa kuwa na uwezo ambao Mungu anamtumia kuliko kawaida kuwaponya wenye shida mbalimbali  ikiwa ni pamoja na matasa, wagonjwa, wenye laana na mikosi, nakila tatizo sugu katika maisha ya wanadamu’’
Fatilia kitakacho jili kwenye blog yetu vbfans1.blogspot.com uweze kujua safari ya uponyaji wa kijana Japhet ndani ya kanisa la Bonde la Baraka kwa Mataifa yote.
Wasiliana na Askofu kwa email revdao@hotmail.com au tembelea Tovuti yetu vbfans1.blogspot.com






0 comments: